SUALA la kusaka watumishi hewa limeendelea kushika kasi nchini baada
ya mikoa kadhaa kutangaza kuikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) kuchunguza kwa kina huku watendaji waliohusika
wakisimamishwa kazi.
MACHO na masikio ya wananchi yameelekezwa leo bungeni kusikia jinsi
Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na
Walemavu inavyowasilisha makadirio ya bajeti.
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema Watanzania milioni 2.3 kati
ya watu milioni 22.3 ambao ndio nguvu kazi ya taifa hawana ajira.
Kiwango hicho cha ukosefu wa ajira kwa mujibu wa NBS ni sawa na asilimia
10.3 ya nguvu kazi ya taifa. Kiwango hicho kinaelezwa kuwa kimepungua
kutoka asilimia 11.7 ya mwaka 2006.
MAGONJWA yasiyoambukiza kwa sasa yameongezeka ukilinganisha na
magonjwa yanayoambukiza hasa magonjwa ya moyo pamoja na mishipa ya damu.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Serikali,
Profesa Mohammed Kambi wakati wa Mkutano wa wadau wa magonjwa ya moyo
kwa nchi za Afrika.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ameahidi kuvaa viatu vya
mtangulizi wake, Paul Makonda kuhakikisha ufisadi unakuwa historia
wilayani kwake. Alisema hayo jana jijini hapa baada ya kuapishwa kuwa
Mkuu wa wilaya hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa na Makonda aliyeteuliwa
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
DIWANI wa Kata ya Kiwalani, Mussa Kafana (Cuf), ameibuka mshindi
katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kumbwaga
mpinzani wake kwa kura nne. Uchaguzi huo ulifanyika jana katika ukumbi
wa Karimjee, baada ya madiwani wa jiji hilo, ambao pia ni wajumbe wa
Baraza la Halmashauri ya jiji hilo kuapishwa.
WATUMISHI wote wa umma wameagizwa kujaza Mikataba ya Mfumo wa Kupima
Utendaji Kazi kwa Uwazi (OPRAS) kuanzia mwaka mpya wa fedha wa 2016/17
na taasisi za Serikali ambazo zitashindwa kutekeleza agizo hilo,
zitatozwa faini.
KIWANGO cha pensheni kwa wastaafu walio kwenye mifuko mbalimbali ya
hifadhi ya jamii waliokuwa wakilipwa kima cha chini Sh 50,115
kinatarajiwa kuongezwa kwa asilimia 100 hadi Sh 100,125.
No comments:
Post a Comment